The House of Favourite Newspapers

Uwoya na skendo kuiba waume za watu

0

MWANAMAMA mkali kunako Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krish’ amefunguka kuwa, hakuna jambo la kishamba kwa sasa kama mwanamke kuiba mwanaume wa mwenzake. Amesema anashangaa wanaofanya hivyo kwani wanaume wapo wengi, ni kiasi cha kujichagulia tu.

Uwoya ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, akimsikia mwanamke akilalamika kuibiwa mwanaume au mwingine akilalamikiwa kuiba mume wa mtu, atamshangaa kwa sababu hayo ni mambo ya kizamani.

Amesema kwa upande wake, kwa sasa huwezi kusikia skendo yake ya kuiba mume wa mtu.

“Kwanza sasa hivi skendo ya kuiba mume wa mtu ni ushamba. Kwanza sijui kama hivyo vitu vipo hadi leo. Mimi huwezi kusikia nina skendo ya kuiba mume wa mtu maana wanaume ni wengu, ni kiasi cha kujichagulia tu,” anasema Uwoya ambaye hivi karibuni alidaiwa kuchukuliwa mwanaume wake na shoga’ke, Katesia Abdul ‘Tessy Chocolate’.

STORI: IMELDA MTEMA

Leave A Reply