
Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Baba duniani tarehe 21 june 2020, EFM redio imezidi kutambua na kuthamini mchango wa Baba au Mzazi wa kiume katika familia.
Hatua hii imekuja baada kutambulisha Kampeni yake mpya iitwayo MSHUA MASTA, ambapo ni jukwaa lililobuniwa na EFM na TVE katika kuonyesha, kuthamini, jitihada za baba katika familia na Taifa. Dira kuu ya jukwaa hili ni kuongeza ushiriki wa wanaume katika mijadala na masuala muhimu ya ustawi wa jamii, Afya na uchumi.
Kampeni hii imemlenga na kumwangazia Baba ama mzazi wa kiume, ambaye anasimama kwa hali na mali katika kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa ajili ya familia na jamii kwa ujumla.
Katika utekelezaji wa kampeni hiyo, EFM Radio imeweza kuhusisha wadau mbalimbali wakiwemo wasanii, wanasiasa, waelimisha jamii na wengineo ambao wanatoa mitazamo yao juu ya kile kinachoonekana juu ya nafasi ya Baba katika jamii, huku wengi wao wakionyesha umuhimu wake kama nguzo katika familia na jamii kwa ujumla.
Vilevile kampeni hii imeangazia sifa zote za baba ambaye anafaa kuitwa MSHUA MASTA ambazo ni mtafutaji mwenye nidhamu ya fedha, Mgawaji wa michongo, Mwenye taarifa kuhusu afya ya uzazi, aliye mstari wa mbele kwenye vita juu ya magonjwa husuani virusi vya UKIMWI (VVU), mwenye kujali na kutetea familia.
Lengo la kuorodhesha sifa hizo ni kumpa hamasa mwanaume ambae ni baba kutambua majukumu yake kwa kuwa mstari wa mbele kuyatimiza.
Kampeni ya MSHUA MASTA inafanyika kwa ushirikiano wa Efm Radio na TVE na Jukwaa la NAWEZA, TACAIDS na DUME CONDOMS (Dume Extreme na Dume Desire)