×

Shikalo Amtaja Jerry Muro Ujio Wake Bongo – Video

UNAAMBIWA kuwa ujio wa mlinda mlango wa Yanga raia wa Kenya, Farouk Shikalo, Bongo umeratibiwa kwa asilimia kubwa na Serikali ya Kenya kwa kushirikiana na Tanzania.

 

Inaelezwa kuwa, msaada wa kumpenyeza mipakani hadi kufi ka Tanzania ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro pamoja na Naibu Gavana wa Mombasa, William King.

Hivi karibuni, Shikalo alirejea Tanzania na kujiunga na Yanga akitokea Kenya kwa usafi ri wa gari baada ya ndege kuzuiwa wakati huu wa janga la corona.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Shikalo alisema: “Safari yangu ya kurejea Bongo ilikuwa ni kama muvi, maana hakukuwa na ndege inayopaa kutoka Kenya kutokana na anga kufungwa kwa tishio la virusi vya Corona, hivyo ilinilazimu nivuke boda kutoka Mombasa mpaka Namanga kwa kuungaunga magari.

 

“Kusema kweli safari yangu ilikuwa na vizuizi vingi lakini haikuwa kazi kwangu kutokana na kusaidiwa na viongozi wa Serikali, baada ya kufi ka mpaka wa Namanga, nilipata changamoto kubwa ndipo Jerry Murro alipata taarifa zangu na kunisaidia kuvuka hadi Arusha.”

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA NA MUSA MATEJA

Leave a Comment