
KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameahidiwa kupewa kiasi cha pauni 1m (Sh Bil 2.9 za Kitanzania) na bonasi nyingine endapo tu atafanikisha timu hiyo kumaliza msimu huu ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo na kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Man United inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Premier ikiwa na pointi 45, imepitwa pointi tatu na Chelsea iliyopo nafasi ya nne.
Solskjaer katika mkataba wake na United, kulikuwa na vipengele vingi vikiwemo vile ya kupewa bonasi ambapo mojawapo ni kuhakikisha timu hiyo itacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hivyo kama atafanikiwa kuingia top four, Solskjaer atapewa bonasi yake ya kiasi cha pauni milioni moja.
Ikumbukwe kuwa, wakati Premier ikirejea, Juni 19, mwaka huu Man United itacheza dhidi ya Tottenham.