Mbunge wa Jimbo la Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Urais wa #Zanzibar. Dkt. Mwinyi amechukua fomu hiyo mchana wa leo katika Ofisi ya CCM Kisiwandui, Unguja.