×

Rais Burundi Kuapishwa Leo, Mama Samia Kuhudhuria!

EVARISTE NDAYISHIMIYE Rais mteule wa Burundi anatarajiwa kuapishwa leo Alhamisi, Juni 18, 2020, badala ya Agosti 2020 kama ilivyopangwa hapo awali.

 

Tume ya Uchaguzi ya Burundi wakati wa mchakato wa uchaguzi, ilileleza kwamba Rais atakayechaguliwa angeapishwa Agosti lakini Mahakama nchini humo iliagiza Rais huyo kuapishwa haraka kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Rais, Pierre Nkurunziza.

 

Ndayishimiye anayetokea chama tawala wa CNDD-FDD, ataapishwa katika Mji wa Gitega ikiwa ni wiki moja baada ya mtangulizi wake kufariki dunia kwa mshtuko wa moyo.

 

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Burundi kuhudhuria sherehe za kuapishwa Ndayishimiye leo.

Leave a Comment