×

Zee Wa Bwax Afungukia Dullah Makabila Kumuimba Vibaya

MSANII wa Singeli hapa nchini Mohammed Rashidi ’Mzee wa Bwax’ wengi wanapenda kumuita mtoto wa nje ya ndoa, amefunguka na kutoa la moyoni kuwa hawezi kumzuia Dullah Makabila kumuimba vibaya kwenye baadhi ya nyimbo zake.

 

Akizungumza na gazeti la Amani, Mzee wa Bwax amesema kuwa ni kweli Makabila amekuwa akimuimba kwenye nyimbo zake, kwa upande wake yeye anachukulia ni kawaida kwa sababu kila msanii anastaili yake ya uimbaji.

 

“Siyo kwamba simsikii Dullah Makabila anavyoniimba vibaya kwenye nyimbo zake, ila mimi siwezi kumzuia, sababu kila msanii huwa anakuwa na staili yake ya uimbaji.

 

 

Yeye kaamua kuja na staili ya kuimba watu, muache aimbe ndivyo vinavyompa mashabiki,” alisema Mzee wa Bwax.

Leave a Comment