×

MC Pilipili Achekelea Mtoto, Mwijaku Aumbuka

KOMEDIANI matata Bongo, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’, amechekelea kupata mtoto huku rafiki yake ambaye ni mwigizaji wa Bongo Movies, Burton Mwemba ‘Mwijaku’ akiumbuka.

 

Pilipili ambaye ni mshereheshaji (MC) maarufu Bongo, ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, anamshukuru Mungu kwa kupata mtoto wa kike aliyempa jina la Elphina aliyezaa na mkewe, Philomena Thadey ‘Cute-Mena’, Ijumaa iliyopita.Mtoto huyo alizaliwa saa 4:00 kamili asubuhi katika hospitali moja iliyopo Msasani jijini Dar.

 

Kabla ya Mungu kumjaalia MC Pilipili mtoto huyo, baadhi ya watu walisema mengi akiwemo Mwijaku aliyetamka waziwazi kuwa jamaa huyo hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.Kwa mujibu wa Mwijaku, MC Pilipili hawezi kumpa mkewe mimba kutokana na ajali aliyoipata miaka ya nyumba mkoani Dodoma.

 

“MC Pilipili hana uwezo wa kumpa mkewe ujauzito kutokana na ajali aliyoipata ambayo ilimharibu mfumo mzima wa uzazi,” alikaririwa Mwijaku.

MC Pilipili aliliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA jana kuwa, hakuna mtu ambaye hatamani kuitwa baba kwenye hii Dunia.Alisema kuwa, anamshukuru mno Mungu kwa zawadi hiyo, japokuwa kuna baadhi ya watu walimsema vibaya kuwa, hana uwezo wa kumpatia mkewe ujauzito, lakini hakukata tamaa na kwa mara ya kwanza anaitwa baba.

 

“Kiukweli ninamshukuru sana Mungu kwa zawadi hii aliyoniletea, najua hakuna mtu asiyetamani kuitwa baba kwenye dunia hii.

 

“Mimi nilisemwa sana kuwa sina uwezo wa kumpa mwanamke mimba, lakini leo Mungu amewadhihirishia wale wote walionisema vibaya.

 

“Kingine wale wanaume wenzangu ambao bado hamjapata watoto, msikate tamaa,” alisema MC Pilipili.Alipotafutwa Mwijaku ili kusikia anasemaje baada ya MC Pilipili kupata mtoto, simu yake iliita bila kupokelewa, hivyo jitihada zinaendelea.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR

Leave a Comment