
Mkuu wa mpango huo, Shakila Mayumana akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Taasisi ya Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) leo imeendesha mafunzo kwa wanahabari kuhusiana na kuichambua bajeti ya serikali iliyopitishwa hivi karibuni katika mrengo wa kijinsia.
Katika bajeti hiyo yalijadiliwa mambo kadhaa ikiwemo sekta ya elimu, afya, kilimo na nyinginezo.
Wanahabari hao walielekezwa jinsi ya kuripoti habari zao kwa kuzingatia mrengo wa kijinsia ikiwemo kuichambua bajeti katika mrengo huo.



HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL