
MABOSI wa Yanga kama wakifanikiwa kupata saini ya kiungo mkabaji wa Slavia Mozyr ya nchini Belarus, James Kotei basi timu hiyo itaachana na Mkongomani, Papy Tshishimbi.
Yanga inaelezwa kuwepo kwenye mazungumzo na kiungo huyo anayemudu kucheza nafasi zaidi ya moja ikiwemo beki wa kati na pembeni kwa ajili ya kuichezea timu hiyo msimu ujao.Timu hiyo imepanga kukisuka kikosi chake katika kuelekea msimu ujao kwa kuziboresha baadhi ya nafasi ikiwemo ya kiungo mkabaji, beki wa kati, pembeni na ushambuliaji.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, Yanga imefi kia hatua hiyo ya kuhamishia nguvu kwa Kotei kutokana na kutoelewa hatima ya Tshishimbi kuendelea kubakia kukipiga Jangwani katika msimu ujao.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kiungo huyo ana zaidi ya mwezi mmoja amepewa mkataba kwa ajili ya kuusaini ambao hadi hivi sasa hajausaini na kufi kia muafaka wa kuachana naye hadi pale atakapotaka mwenyewe asaini.
Aliongeza kuwa wakati Yanga ikimuweka kando Tshishimbi, mabosi wa timu hiyo wapo kwenye mazungumzo mazuri na Kotei ambaye inaelezwa huenda akatua Jula 10, mwaka huu kusaini mkataba wa miaka miwili kabla ya kutangaza kuachana na Mkongomani huyo.
“Yanga kama ikifanikisha mipango yao ya kumsajili Kotei, basi utakuwa mwisho wa kiungo wao Tshishimbi ambaye anausumbua uongozi wa timu hiyo baada ya kugomea kusaini mkataba aliopewa wa miaka miwili.
“Mabosi hao wanaipambania saini ya Kotei anayeelezwa huenda akatua nchini kuja kusaini Yanga Julai 10, mwaka huu mara baada ya kufi kia muafaka mzuri kwa dau ambalo analitaka.
“Viongozi hao wa Yanga wapo katika hatua nzuri za kukamilisha usajili wake baada ya Kotei kuvunja mkataba wa kuendelea kuichezea klabu yake hiyo ya Slavia Mozyr,”alisema mtoa taarifa huyo.
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi waUwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, alisema: “Katika usajili tuko makini mno kwenye eneo hilo, mpaka sasa tumeshasajili wachezaji wapya watano, wawili wanatokea hapa ndani ambapo kuna winga na beki, sitapenda kuwataja majina yao.”
Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam