
Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaruhusu waendesha pikipiki (bodaboda) kuingia sehemu yoyote ya jiji la Dar es Salaam ikiwa wamefuata taratibu za kuwa na leseni, kuvaa kofia ngumu na kufuata sheria za barabarani.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaruhusu waendesha pikipiki za usafiri (bodaboda) na madereva wa Bajaj kuingia sehemu yoyote ya jiji hilo mradi wawe wamefuata taratibu zinazotakiwa, ambazo ni pamoja na kuwa na leseni, kuvaa kofia ngumu.

“Bodaboda pamoja na Bajaj nawaruhusu kuingia popote hadi katikati ya mji na ikiwa kuna yoyote amekukamata mwambie Makonda ametoa kibali cha mimi kuingia huku ili kujitafutia kipato,” alisema Makonda.
Aidha alisema kuwa jumla ya Shilingi bilioni 500 zimeshatolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mitaa mbalimbali za jiji hilo.
“Tunamshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa sababu tayari ameshatoa fedha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 111 katika Wilaya hii,” alisema.
Akizungumzia kuhusu mikopo iliyotolewa na manispaa ili waweze kuwakopesha kina mama, vijana na walemavu, amesema mikopo hiyo inatolewa na hairudishwi kwa riba, ili iweze kuwasidia wahusika.

“Na pia tayari mikopo imeshatoka ya shilingi bilioni 33 ambapo manispaa ilitoa kwa ajili ya kuwakopesha kina mama, vijana na walemavu lakini hazijawafikia; sasa nawaagiza Takukuru wachunguze kama fedha hizo zimewafikia wahusika ama la,” alisema.
Baadhi ya miradi iliyokabidhiwa ni pamoja na jengo lilipo katika Hospitali ya Palestina Sinza na soko lililopo neo la Mawasiliano.