
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasika na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu, amesema atarejea Tanzania mwishoni mwa mwezi huu (Julai) ili kuendelea na shughuli mbalimbali za kisiasa
Amesema atahudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Chama unaotarajiwa kufanyika Julai 29. Mkutano huo utampitisha mgombea urais wa chama hicho kwenye uchaguzi kuu mwaka huu (2020).
Lissu amekuwa nje ya nchi tangu Septemba 2017 na hii itakuwa mara ya kwanza kwa mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki kurejea nchini tangu ashambuliwe na watu wasiojulikana jijini Dodoma
Mbali na Lissu, watia nia mwengine wa Chadema ni Freeman Mbowe, Peter Msigwa, Lazaro Nyalandu, Isaya Mwita, Nikodemus Gaspar, Naro Opio, Richmund Simba, Shabani Msafiri, Dkt Majinge Maryrose, Manyama Leonard.