×

Sven: Yanga? Ngojeni

KIWA imebaki wiki moja kabla ya Simba na Yanga hazijapambana katika mchezo wa nusu fainali wa Kombe la FA, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameweka wazi kwamba muda wa kuiwaza mechi hiyo bado haujafi ka.

 

Kocha huyo amefunguka kwamba, amewaweka ‘kiporo’ Yanga kutokana na akili yake kwa sasa kuwaza mechi mbili za Ligi Kuu Bara zilizo mbele yake kwani anataka kushinda hizo kwanza licha ya kwamba tayari wamekuwa mabingwa.

 

Sven amesema lengo lake kabla ya mechi hiyo ya Julai 12 itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar ni kushinda mechi dhidi ya Jumatano ijayo dhidi ya Namungo, zote zikiwa ugenini.

 

“Kuhusiana na mechi na Yanga, itakuwa ngumu kwa timu zote mbili, lakini kwangu kwa sasa siyo muhimu. Kuna siku zaidi ya nane kabla ya mechi hii, hivyo basi siwafi kirii sana.

 

“Kwa sasa kilicho mbele ni kuangalia namna gani tunashinda mechi zetu za ligi. hatutaki kuona tunakosa pointi kwenye mechi hizo licha ya kwamba tumekuwa mabingwa,” alisema Sven.

SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave a Comment