×

Mambo ya Kapombe Magumu, Aikosa Yanga

BEKI kiraka wa Simba, Shomari Kapombe hataonekana tena uwanjani kwenye timu hiyo msimu huu.Kiraka huyo alipata maumivu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliowakutanisha Simba na Azam FC uliopigwa wiki moja iliyopita baada ya kuchezewa vibaya na kiungo Frank Domayo.

 

Kapombe tayari amekosa mchezo mmoja wa ligi waliocheza na Ndanda FC, uliopigwa Nangwanda Sijaona huko mkoani Mtwara kabla ya leo kucheza mwingine dhidi ya Namungo FC na anatarajiwa pia kukosa mchezo wa Jumapili dhidi ya Yanga kwenye FA.

 

Kwa mujibu wa daktari mkuu wa timu hiyo, Yassin Gembe beki huyo baada ya kufanyiwa kipimo cha MRI, ameonekana kupata majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne.

 

Gembe alisema kuwa beki huyo alifanyiwa vipimo hivyo kwenye hospitali ya Muhimbili.Aliongeza kuwa beki huyo baada ya majibu ya vipimo hivyo hivi sasa anaendelea matibabu huku jopo la madaktari wa timu hiyo wakimweka chini ya uangalizi ili kuhakikisha kabla ya ligi awe amepona tayari kuipambania timu yake.

 

“Kapombe hatakuwepo katika sehemu ya kikosi chetu katika michezo tuliyoibakisha ya ligi na Kombe la FA ni baada ya vipimo vya daktari kutoka kwa madaktari kuonyesha kuwa hawezi kuwa fi ti hivi karibuni.

 

“Majibu ya MRI yaliyotoka baada ya kipimo hicho ameonekana kupata majeraha katika sehemu ya goti lake, hivyo atatakiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne.

 

“Kama unavyofahamu ligi imebakia kama wiki mbili ili imalizike, hivyo hadi ligi inamalizika Kapombe anakuwa bado hajapona, kama kuonekana ataanza kuonekana msimu ujao,” alisema Gembe.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Timiza malengo yako leo kwa kutuma dau lako 500-2000 kwenda namba ya kampuni 551551 kumbukumbu namba weka namba zako 5 za ushindi zikifuatiwa na neno SHINDA. Mfano 12345 SHINDA

#ChezaPesaShindaPesa #SioKawaida#chezaglobal

DEWJI ATAKA SIMBA, YANGA IAHIRISHWE, BANKA ATUA BUKOBA KABLA YA KUIVAA SIMBA


 

Leave a Comment