×

Waoo..! kama jana vile!-22

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:

Mama Monica na Magembe walizama kwenye mechi, mama Monica kama kawaida yake alianza mbwembwe za mahaba kiasi cha kelele zake kufika nje kwa wale vijana hali iliyowalazimu waanze kuweweseka.

Magembe alikuwa anaongeza spidi na kupunguza, anaongeza na kupunguza. Wale vijana nao wakawa wanakwenda naye sambamba lakini walitaka sana Magembe akaze mwendo ili wao wamalize…

“Bro si uongeze spidi moja kwa  moja tu ijulikane moja.”

JIACHIE MWENYEWE…

Mama Monica alimsukuma Magembe mpaka akafika kwenye kona ya chumba kisha yeye akaiwahi swichi ya taa ukutani… tap! Akaizima!

Nje kukasikika kishindo cha watu kukimbia. Wale vijana waliondoka kwa mbio huku wakisikika wakisema…

“Jamaa poa sana,  lakini demu noma…”

Mama Monica alipotoka kuzima taa, alikwenda kitandani na kukaa, akamuita Magembe…

“We Magembe.”

Wakati huo, Magembe yeye alikuwa amesimama palepale kwenye kona ya chumba baada ya kuondolewa uwanjani bila mwenyewe kupenda wala kujadiliana na alikuwa anapiga pasi kuelekea kwenye ushindi…

Ilibidi asogee hadi alipo mama Monica, akakaa…

“Sema…”

“Unajua kuna kitu nimejifunza kutoka kwako Magembe!”

“Kitu gani hicho?”

“Wewe na hawa vijana mlikuwa na njama moja.”

“He! Njama kama ipi?”

“Kunichora mimi.”

“He! Mama Monica… mimi nawajulia wapi hawa vijana? Si tumekuja pamoja mimi na wewe! Niliposema twende gesti ile tuliyoizoea, wewe ukakataa. Ukasema unaweza kukutana na kaka yako…ukasema tutafute kwingine. Wakati nafuta hapa wewe upo…sasa hawa vijana mimi ningewatoa wapi?”

Kwa mbali, mama Monica alionekana kukubaliana na Magembe, lakini bado alikuwa ana maswali…

“Sasa kwa nini wakati wanaondoka wakasema, ‘jamaa poa sana,  lakini demu noma’..?”

“Hata mimi sijui ni kwa nini walisema hivyo kwani labda ni watu waliozoea kufanya tabia hii na kukuta wanaume hawashtuki sana kama wanavyoshtuka wanawake.”

Wawili hao hawakuwa na namna, waliamua kuendelea na mechi yao lakini huku kukiwa na giza jambo ambalo mama Monica aliliona linamfanya kuwa huru zaidi.

Magembe alipojaribu kumshawishi wawashe taa, mama Monica alikuja juu akisema haitatokea tena kuingia kwenye gesti hiyo na kuwasha taa.

Hapo kama ilivyokuwa awali, walisakata mechi lakini si kwa kuingia uwanjani bali nje kwa kuogopa kunguni…

“Unajua wale vijana wamenifaidi sana kama kweli walikuwa wananichungulia. Na lazima walikuwa wanatuchungulia. Yaani wameona mambo yangu yote nikiwa kitandani, wakiniona kesho si watanicheka?” alisema mama Monica, Magembe akamtuliza…

“Hakuna atakayeweza kukuona kesho akakumbuka. Huu ni usiku bwana. Mambo ya usiku yanakuaga kiusikuusiku.”

“Mh! Unasema tu wewe…”

Basi, kwa shidashida hivyohivyo, wakajikuta wote wanapata ushindi wa sare lakini hakuna aliyekuwa tayari kuendelea na mechi kutokana na mazingira.

Mama Monica alimwomba Magembe kumsindikiza kwenye choo cha nje. Alipotoka alijiandaa, wakatoka huku Magembe akimfuata mhudumu na kumuwakia…

“Wanakujaje vijana kutuchungulia na nyie mpo? Halafu kwa nini milango yenu ina nyufa mpaka mtu anaona ndani? Pia ni kwa nini pazia zenu ziko nusu dirisha?”

“Broo ukitoka nje, angalia bango la jina la hii gesti linasemaje  ndiyo uanze kulaumu,” alisema mhudumu wa gesti hiyo iliyopo uchochoroni sana.

Magembe alihisi kushindana au kupigizana kelele na mhudumu huyo ni sawa na kuzozana na mlevi. Aliamua kutoka akiwa anafuatwa kwa nyuma na mama Monica.

Walipotoka nje, waliangaza juu kutafuta, wakakutana na bango la jina la gesti; UTARATIBU SIFURI GUEST HOUSE.

Kwanza Magembe alicheka, mama Monica naye akacheka, Magembe akauliza…

“Hivi ni kwa nini hili bango hatukuliona?”

“Na mimi nashangaa, sijui ni kwa nini!”

Mbele kwa mbele, walisimama ili kuagana, Magembe huku akikumbuka ahadi ya kesho yake kwenda kupima Ukimwi, aliamua kumpa pesa nyingi mama Monica kama kumchanganya akili.

Magembe alijua ameshamwambukiza virusi mwanamke huyo na akajua kwa vile kaka yake alishawaona gesti, yeye kukwepa msala si rahisi…

“Sasa kesho usisahau ahadi ya kwenda kupima virusi,” alisema mama Monica wakati Magembe alishaliweka wazo hilo akilini mwake.

“Ahadi iko palepale baby…hizi senti zitakusaidia siku mbili hizi,” alisema Magembe huku akimkabidhi kitita cha pesa mama Monica ambaye alishtuka kuona mzigo ni mkubwa. Moyoni akasema…

“Itakuwa mia tano mia tano.”

Mama Monica akabadilika akili, akaachana na habari za kusisitiziana kuhusu kesho yake, akamshukuru sana Magembe na kumbusu…mmmwaaa!

Mama Monica aliziingiza zile pesa kwenye kipochi chake. Aliposhuka akawa akitembea kwenda kwake, akatumia nafasi hiyo kuzihesabu zile fedha, moja baada ya nyingine. Kwanza aliziangalia akagundua ni shilingi elfu kumikumi…

“Kumi…ishirini…thelathini…arooobaini…hamsiiini….siiitini…sabini…themaaanini…tisiniiii…laaaki…laki na kuumi…”

Moyo ulimlipuka mama Monica kwani alihesabu mpaka akafikia shilingi laki tatu na bado mkononi alikuwa na nusu nyingine na hapo alikuwa ameshakaribia kuingia nyumbani kwake…

  “Ina maana kama hizi ni laki tatu na huku ninazo kama hizi, ina maana hizi ni laki sita,” alisema moyoni na kujikuta akijiogopa mwenyewe…

“Inawezekana kweli?” alijiuliza.

Aliingia ndani kwake, akamkuta mumewe sebuleni…

“Umechelewa sana mama Monica.”

“Ni kweli mume wangu, kulikuwa na wateja sana leo,” alisema mama Monica huku akiweka ule mkoba juu ya meza huku akivua sendozi. Kumbe alikuwa hajafunga zipu, zile shilingi laki sita zote zikatoka na kusambaa sakafuni.

Leave a Comment