×

Vifusi Vyageuka Kero kwa Madereva Buchosa – Sengerema

 

 

Moja ya magari yanayofanya shughuli za usafirishaji kati ya Bukokwa na Luchili, Buchosa, mkoani Mwanza,  yakipita eno hilo kwa shida kutokana na kulundikana kwa vifusi ambavyo havijazambazwa kwa muda mrefu.

VIFUSI vya mchanga katika Halmashauri ya Buchosa – Sengerema mkoani Mwanza vimegeuka kuwa kero kwa madereva baada ya kulalamikia kuwa ni muda mrefu sasa vimerundikwa pasipokusambazwa na kusababisha kuwa kero kwa waendeshaji wa vyombo vya moto hususan magari na pikipiki.

Baadhi ya vifusi ambavyo vimekuwepo muda mrefu barabarani bila kusambazwa.

Baadhi ya madereva waliozungumza na mtandao huu wameeleza kuwa vifusi hivyo vimerundikwa maeneo ya Bukokwa hadi maeneo ya Luchili ambapo kuna umbali wa takribani kilomita nne hadi tano.

Wameelezea kuwa vifusi ni kikwazo kikubwa hasa wakati magari yanapopishana ambapo hujikuta yakikwama mitaroni.

“Tunaiomba serikali itusaidie hasa kwa mamlaka zinazohusika kuvisambaza vifusi hivyo ili kutuondolea adha hiyo.  Ni muda mrefu tangia vimekuwepo lakini hatuoni juhudi zozote za kuvisambaza,  hivyo tunaiomba serikali kutilia mkazo suala hilo ili magari yaweze kupita kwa urahisi,” alieleza mmoja wa madereva wanaofanya shughuli za usafirishaji maeneo ya Nyakaliro na Sengerema aliyejitambulisha kwa jina la Paul Maduka.

Leave a Comment