BAADA ya kupona homa ya Covid-19 inayosababisha na virusi vya Corona, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, ametoa wimbo maalum kwa ajili ya shukurani kwa Mungu huku akiendelea kuwasisitiza Watanzania kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo ambavyo vinaendelea kuitesa dunia na kutikisa zaidi mataifa ya Amerika.