
JE, Diamond na Zari wamerudiana? Wawili hao wamekuwa katika mahusiano mema hivi majuzi baada ya Diamond na Zari kukosana na msanii huyo kukataa kuwasaidia watoto wake kwa zaidi ya muda wa miaka miwili.
Diamond alianza kuzungumza na wanawe na kisha kuwasaidia, baaada ya Zari kupitia kwenye mitandao ya kijamii kusema kuwa hawasaidii wanawe ambao ni Tiffah na Nillan aliozaa na Mganda huyo ambaye kwa sasa anaishi kwake nchini Afrika Ksuini.
“TWO YEARS DOWN THE LINE DIAMOND REALISED WHAT HIS MISTAKE WAS WHERE HIS PROBLEM WAS AND HE SAID, HE IS NOT GONNA LET THIS CONTINUE AND HE DECIDED TO BE IN HIS KIDS’ LIFE. SO HE STEPPED UP, WHY CAN’T I GIVE CREDIT FOR THAT?” Aliandika Zari.
Siku ya kusherehekea Siku ya akina Baba Duniani, Zari aliposti picha mtandaoni huku akimwonyesha Diamond mapenzi tele, awali kupitia kwenye mitandao ya kijamii Zari aliposti picha ambayo iliwaacha wengi wakizungumza na kuulizana maswali yasiyo na majibu. Mama huyo wa watoto watano alimshukuru aliyekuwa mumewe huku wengi wakisema Diamond alimsaidia kununua gari hilo.
“ASANTE BABA T FOR THE TOP-UP,” Aliandika Zari.
Je, Diamond ndiye alimtumia pesa kununua gari hilo au mambo vipi?