The House of Favourite Newspapers

Jamaa Wazidi Kumkazia Meek Mill

0

JAMAA wa Kampuni ya Dream Rich Entertainment wamezidi kumkazia kinoma staa wa muziki wa Marekani, Meek Mill kwa madai ya kuiba mashairi na kuyatumia kwenye ngoma zake.

Dream Rich ambayo ni lebo ya muziki kutoka pande za Philadelphia, Marekani imemfungulia Meek Mill mashtaka hayo kwa ukiukaji wa hakimiliki akidaiwa kuiba mashairi kutoka kwa mtunzi ambaye aliunganishwa naye kupitia lebo hiyo.

 

Meek Mill anadaiwa alipata nafasi ya kuingia kwenye mafaili ya mtunzi huyo na kujipakulia mashairi ambayo aliyatumia kwenye ngoma zake za 100 Summers na Cold Hearted II ambazo zipo kwenye album yake ya Championshipsbila ridhaa ya wahusika.

Dream Rich wanadai fidia ya Dola za Kimarekani 300,000 (zaidi ya shilingi milioni 695 za Kibongo).

STORI: PHILADELPHIA, MAREKANI

Leave A Reply