×

Unasumbuliwa na Maumivu ya Kiuno, Mgongo, Mifupa? Soma Hapa

WATU wanaofanya shughuli nzito zinazohitaji nguvu kubwa za mwili ikiwemo kubeba mizigo mizito na zile zinazohusha kuinama au kuchuchumaa kwa muda mrefu, wanakabiliwa na tatizo kubwa la maumivu ya mgongo, kiuno au wakati mwingine miguu kufa ganzi.

Wanamichezo nao wanakuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa yanayoshambulia viungo mbalimbali vya miili yao, bila kuwasahau askari, hasa wale wanaofanya kazi za kusimama muda mrefu ikiwemo gwaride.

Kitaalamu inaelezwa kwamba magonjwa mengi yanayoshambulia kiuno, mgongo na mifupa ya mwili, huwa yanasababishwa na kuvipa viungo hivyo mzigo mkubwa mara kwa mara.

Wapo wafanyakazi ambao kutokana na kazi zao inawabidi kuchuchumaa kwa muda mrefu, kupindisha viungo vyao hasa miguu kwa muda mrefu na kuna kazi nyingine huleta madhara ya viungo kuumia kazini kwa mfano kwenye michezo, kwenye ajali, kuanguka na kadhalika.

Habari njema ni kwamba dawa ya Life pamoja na Rise Up zinazotengenezwa na Kampuni ya KJRBS chini yake Mkurugenzi Tabibu Riziki Nkya, zimetengenezwa kwa mitishamba na zina uwezo wa kutibu matatizo mbalimbali yakiwemo yaliyotajwa hapo juu.

Baadhi ya magonjwa hutatiza utendaji kazi wa mhusika na hata kumpotezea nguvu za kufanya kazi. Madhara anayopata mwanadamu katika viungo vya kuanzia kiunoni hadi kwenye nyayo ni pamoja na kupata maumivu ya kiuno, nyonga, miguu na magoti na kwa kawaida hutokana na kutumiwa kupita kiasi kwa viungo hivyo.

Wafanyakazi mara nyingi hulalamika kuumwa na viungo hivyo na kupata ganzi hata bila kuwa na magonjwa yoyote wanayougua. Magonjwa yanayosababishwa na madhara makubwa yanayoletwa na matukio ya ghafla kama vile ajali si kawaida kutokea na kusababisha madhara hayo, lakini wanariadha na wanajeshi hukabiliwa na aina hii ya madhara.

Hawa pia wanashauriwa kutumia dawa ya Life ambayo ni bora, haina kemikali kwani imetengenezwa kwa mitishamba na ni salama kwa afya ya binadamu.

Ushahidi wa kisayansi unaeleza kwamba kuna magonjwa kadhaa yanayoathiri viungo vya chini kuanzia kiunoni, ambayo yana uhusiano na kazi. Magonjwa hayo ni kama vile arthritis ya kiuno na magoti.

Pia kuna magonjwa ambayo yanajulikana kwa lugha za kitaalam kama vile knee bursitis, meniscal lesions/tears na magonjwa mengine yanayoshika sehemu za chini za miguu.

Kwa maelezo mafupi ya magonjwa haya ni kama ifuatavyo: Ugonjwa unaoitwa Osteoarthritis (OA) ni ugonjwa ambao unapokupata huwa hautibiki kwa urahisi na unaendelea kuleta madhara makubwa. Ni ugonjwa unaoshika kiuno nyonga na uti wa mgongo.

Madhara hayo hukupata wakati sehemu ya maungo yanayofunika viungo hivyo yanapoharibika ama kuisha. Magonjwa haya ya nyonga yanawasumbua zaidi wanaume kuliko wanawake, na wakulima wako katika hatari kubwa ya kuathirika kwa asilimia kubwa na ugonjwa huo. Nao pia wanashauriwa kutumia dawa za Life pamoja na Rise Up.

Kundi jingine la wafanyakazi ambalo lipo katika hatari ya kupata magonjwa haya ni pamoja na wafanyakazi wa migodini, mafundi wa sakafu kama wale wanaoweka “tiles” majumbani, na wanaofanya kazi za kusafisha sakafu.

Knee bursitis ni ugonjwa ambao umebandikwa majina mengine kama vile ugonjwa wa wachimba madini, ugonjwa wa waandalizi wa mazulia, na ugonjwa wa magoti wa wafanyakazi wa majumbani.

Ugonjwa huu husababishwa na kuchuchumaa mara kwa mara au kufanya shughuli ambazo zitalifanya goti kulemewa na uzito mara kwa mara.

Wafanyakazi wanaopata ugonjwa huu mara nyingi hupata dalili kama kuvimba magoti na sehemu za magoti kuwa laini, magoti kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi ikiwemo maumivu yanayoweza kumfanya mhusika ashindwe kugeuza goti kwa haraka huku ngozi ya sehemu za goti ikikakamaa na kuwa ngumu.

Pia kuna ugonjwa wa ngozi ya goti kuwa nzito unaojulikana kama Beat knee au hyperkeratosis. Ugonjwa huu unasababishwa na shinikizo kubwa la goti, yaani kulipa kazi za uzito mkubwa. Kwa tatizo hilo tumia dawa ya Life pamoja na Detox Immuno Booster.

Bursitis ni ugonjwa mkubwa unaowaathiri sana wale wanaojishughulisha na kazi zinazolipa goti shinikizo kubwa la kikazi kama vile kupiga magoti na kuchuchumaa. Hawa pia wanashauriwa kutumia dawa ya Life pamoja na Cotex.

Ugonjwa mwingine ni wa Meniscal lesions/tear damage ambao unahusu kupinda au kunyongeka kwa goti wakati mtu anapobeba mzigo wenye uzito mkubwa. Mzigo unapokuwa mzito unaweza kusababisha madhara kwenye goti na kusababisha mipasuko ya sehemu za goti.

Madhara hayo yana uwezo wa kusababisha ugonjwa wa goti kuwa mbaya zaidi na hatua za tahadhari zinapaswa kuchukuliwa mapema iwezekanavyo. Madhara mengine ya goti yanajulikana kama Stress Fracture. Magonjwa haya yanasababishwa na kuyapa magoti mshindo wa kuendelea ambao husababisha mifupa ya miguu kupasuka kidogokidogo.

Magonjwa haya huwapata zaidi wanaofanya kazi za kijeshi kutokana na mazoezi yao ya kutembea kwa kukanyaga kwa kishindo (gwaride). Magonjwa haya yanawasumbua zaidi wanajeshi na wanariadha hasa wale wanaoshiriki riadha za mbio ndefu.

Ili kujikinga na magonjwa haya, tumia dawa ya Fratox na Life pakiti tisa mfululizo.

Kwa maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana na Tabibu Riziki, bingwa wa tiba za magonjwa mbalimbali kwa kutumia dawa za kisasa zilizotengenezwa kwa mitishamba kwa namba za simu 0767352352 au 0744111115, unaweza pia kufika kwenye Ofisi za JKBRS zilizopo Ubungo Plaza, Ghorofa ya Chini jijini Dar es Salaam.

STORI: MWANDISHI WETU, DAR

Leave a Comment