×

Man City Yashinda Rufaa Kufungiwa na UEFA

KLABU ya Man City imeshinda rufaa yake dhidi ya Shirikisho la  Soka Ulaya (Uefa) Club Financial Control Body (CFCB) ambayo iliwafungia kutocheza michuano ya Ulaya kwa misimu miwili kwa kuvunja kanuni za Financial Fair Play (FFP) kati ya mwaka 2012 na 2016.  Mahakama ya Michezo (CAS) imewaondolea adhabu hiyo.

 

Mahakama ya usuluhishi ya michezo imetengua kifungo kwa klabu ya Manchester City cha kutoshiriki mashindano ya Ulaya msimu ujao. Sasa ni rasmi, City watashiriki kwenye msimu ujao wa ligi ya mabingwa ambapo awali walitakiwa kutoshiriki michuano hiyo kwa kipindi cha miaka miwili.

Leave a Comment