×

Watiania wa Ubunge CCM Waliochukua Fomu Leo – Pichaz

Waziri wa Uwekezaji Angela Jasmine Kairuki amechukua fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM leo Julai 14 , 2020. Anayemkabidhi fomu hiyo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Same bibi Victoria Mahembe.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. Jimbo hilo lilikuwa linaongozwa na Halima Mdee (Chadema).

Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini kupitia tiketi ya CCM, Dkt.Tulia amechukua fomu hiyo katika ofisi za CCM Wilaya akisindikizwa na Mume wake James Andilile Mwainyekule.

“Kwa sasa itoshe tu kwamba nimechukua fomu,” amesema Askofu Gwajima muda mfupi baada ya kuchukua fomu.

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amechukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea ubunge kwa tiketi  CCM jimbo la Arusha Mjini, ikumbukwe jimbo hilo limekuwa likiwakilishwa na Godbless Lema katika chaguzi kadhaa na yeye ameshachukua fomu kugombea tena.

Kwenye foleni hiyo, alikuwemo Abbas Tarimba, aliyekuwa kiongozi katika Timu ya Mpira ya Yanga na Diwani wa Kata ya Hananasifu ambaye anaomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Kinondoni.

Mbunge anayemaliza muda wake kwenye jimbo hilo ni, Maulid Mtulia wa CCM.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

 

Abasi Tarimba ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Ananasif, amechukua fomu za kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) kugombea Ubunge katika Jimbo la Kinondoni.

 

 

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo Singida Mashariki Miraji Mtaturu amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, kachukua fomu kuwania ubunge kupitia CCM Jimbo la Karagwe.

 

Leave a Comment