×

Mr. Blue Anapiga Kwa Maneno

STAA wa muziki wa Bongo Fleva; Kheer Samir ‘Mr Blue’, afunguka kuwa yeye si mwanaume wa kumpiga ngumi mkewe, bali anapiga kwa maneno.

 

Akipiga stori na Amani, Mr Blue amesema kuwa yeye hajawahi kumpiga mkewe hata kofi, bali anatumia maneno kumrekebisha.

“Si jambo zuri kumpiga mwanamke, na katika maisha yangu, sijawahi kumpiga mwanamke, ila maneno yangu yanatosha kumchapa,’’ alisema Mr Blue ambaye anafanya poa na ngoma yake ya Mautundu.

 

Ishu ya wanaume kuwapiga wapenzi wao imekuwa hot hivi karibuni baada ya msanii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kuibua tuhuma za kupigwa na mume wake Uchebe, ambapo mastaa kadhaa wamekuwa wakijitokeza na kupinga tabia hiyo

Leave a Comment