×

Zahera Ambakiza Molinga Yanga

ALIYEWAHI kuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, ametoa kauli inayomaanisha kuwa anatamani kuona David Molinga akiendelea kubaki kuichezea Yanga msimu ujao kwa kuwa ni mchezaji mzuri ambaye kiwango chake kinafanana na Meddie Kagere na John Bocco wa Simba.

 

Molinga ndiye kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga baada ya kufunga mabao 10 huku Kagere akiongoza kwa kufumania nyavu kwa kuwa na mabao 19 hadi sasa.

 

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Zahera alifunguka kuwa, Molinga ni miongoni mwa wachezaji wenye kiwango cha juu ndani ya Yanga ambaye anahitaji kupewa nafasi ili aweze kufumania nyavu kwa kuwa kiwango chake kinafanana na Kagere na Bocco.

“Watu wengi wal-isema Molinga hafai, huyu ni mchezaji mzuri anaweza kuisaidia Yanga, kocha ana-takiwa amu-elewe Molinga ni mchezaji wa aina gani, anacheza vipi, ufungaji wake hautofautiani na Kagere na Bocco.“Nilisema atafunga mabao mengi akipewa nafasi atafanya vizuri zaidi, takwimu ya mchezaji ndiyo inayoonyesha kama ni mchezaji mzuri ama mbaya.

 

“Anatakiwa umjue ni mchezaji wa aina gani afanyishwe mazoezi ya kufika ndani ya boksi ili aweze kufunga mabao mengi, alikuwa anawekwa benchi hapati nafasi ya kucheza ndiyo maana alishindwa kuonyesha kiwango chake hapo nyuma,” alisema Zahera.

 

Alimalizia kwa kusema kuwa, Yanga ya sasa ni nzuri ukilinganisha na ile ya kwake kutokana na usajili mzuri ambao umefanywa.Aidha, katika taarifa ambayo Championi Ijumaa imezipata ni kuwa, Molinga ambaye inadaiwa ameshapata timu nyingine ya ku-jiunga nao nje ya Tanzania, ni mion-goni mwa wache-zaji wanaotakiwa kuondoka Yanga akiwa pamoja na Mrisho Ngassa, Andrew Vicent ‘Dante’, Tariq Seif na wen-gine kadhaa.

STORI: Khadija Mngwai,dar es Salaam

Leave a Comment