
KARIBU mpenzi msomaji wa safu hii pendwa ya FASHENI. Wiki hii ninakuletea fasheni ya viatu vikubwa ambavyo vinaweza kuwa ni raba au viatu vya kamba vyeusi almaarufu Buti la Jeje ambalo linatrendi kinoma mjini na mitandaoni.

Licha ya fasheni hii kuvaliwa sana miaka ya nyuma, lakini imekuja kwa kasi baada ya kuvaliwa na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwenye wimbo wake wa Jeje. Hivyo, kuwafanya watu wengine kuvaa viatu vikubwa na wao kuambiwa wamevaa Buti la Jeje.

Uzuri wa fasheni hii ni kwamba, inaweza kuvaliwa na watu wa jinsia zote kwa kutupia pensi, suruali, skin tight, suti, kimini na hata gauni.
Mbali na fasheni hii kuvaliwa kwenye mitoko ya hapa na pale, pia inaweza kuvaliwa ofisini na kutokelezea ile mbaya.