×

Harmonize Dizaini Flani Kama Kashauelewa Muziki

Ni miaka michache imepita tangu msanii Rajab Abdul “Harmonize” wengi wanamuita Konde Boy au Jeshi , atoke rasmi kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), ni kwamba  tunaweza kusema kuwa alikuwa anakuja kwa kupita kama wengi waliyopita , japo kuna wengi waliamini kuwa Harmonize huyu  atabaki kwa Diamond, kama alivyokuwa Rayvanny na Lava lava.

 

PONGEZI KWAKE

Binafsi nampongeza kijana wa Mtwara, Konde Boy kwa mafanikio aliyoyapata sasa hivi ameweza kutengeneza Lable yake mwenyewe ya Konde Music Worldwide”Konde Gang”, na pia amekuwa na uwezo wa kumsimia msanii siyo jambo la kitoto, Harmonize anajielewa siyo kama wasanii wengine wanaamua kutoka kwenye kundi wanaishia kutapatapa huku na kule.

 

Kwa sasa hivi Huwezi kumfananisha Harmonize na Rich Mavoko walivyotoka kwenye label, ikumbuke Rich Mavoko alitoka kabla mkataba haujaisha bado alikuwa hajajijenga kimaisha mpaka sasa kuna uwezekano Rich Mavoko hata pesa vya kulipia video anakosa, alitoka ili kuanza na yeye kusimamia wasanii akajikuta anashindwa kujisimamia hata mwenyewe.

Kwa upande wa Harmonize ukiangalia tayari kajijenga kimuziki na kimaisha sasa kama mtu una mamilioni ya pesa  ndani kuna haja gani tena kuendelea kusimamiwa na kutumikishwa tumwache Harmonize  afanye kazi zake kwa uhuru utoaji wa nyimbo WCB utagundua ni kama kutumikishwa inalazimika mara kwa mara msanii awepo studio na kwenye shoo tofauti na wasanii wakubwa Marekani ambao wapo chini ya Label mwaka mzima msanii unaweza usimsikie.

 

Mungu angempa uwezo wa kujua hili mapema basi Harmonize angekuwa ashafikia level za akina Wizkid na Davido kutokana na jinsi anavyojituma kimuziki, kamanda huyu muda wote anawaza nini cha kufanya  ili muziki wake uendelee kuwa juu.

Huku wasanii wenzake wakiwa bize na Totozi mjini na wanawaza kwenda kula bata Dubai. Harmonize  kwa sasa anasaka pesa kwa kasi kuliko kitu chochote.

 

ASAINI  MADILI MAKUBWA

Harmonize tangu atoke Wasafi amefunguka akili, ambapo kwa sasa anapata tuzo mbalimbali kila siku,hii leo kumlinganisha na wasanii wengine,unahitaji roho ya kijasiri na iliyokosa aibu, Harmonize yupo juu mno, Diamond mwenyewe anakiri kuwa Harmonize hana kazi mbovu mjini.

 

Hapa alipofika wengi wanatamani kuwa kama yeye mfano mkubwa Rayvanny na lava lava, Harmonize ashavua kabisa akili za Kimakonde na anajua kutumia jina lake vizuri kwenye masuala ya  biashara , Harmonize wa sasa siyo yule wa WCB tena.

 

Sasa hivi anapokea Madili makubwa  kama Ubalozi wa Sayona Twist na CRD Bank na mengine tusiyoyajua , anasaini cheki za pesa kila muda na kila wakati.

 

Kila siku anafanya mambo makubwa kwenye muziki ,utadhani ndiyo anatoka kisanii, hasira za gemu la muziki hazijawahi kuisha kichwani mwake, hataki kuwa nyuma ya wenzake kama ilivyokuwa kwa Diamond alitamani kumpita Ali Kiba, na yeye anatamani siku moja aje kuwa kama  AKA NA NYOVEST.

 

“Never Give Up” ni wimbo aliyoimba akiwa anamanisha kwamba usikate Tamaa, mtoto wa mtwara ashawahi kukatishwa tamaa sana, alishawahi kuwa machinga ameosha miguu ya warembo  hapa mjini, aliamua kujiunga na Bongo Star Search(BSS).

 

“ Lakini Madame Ritha na Master J walimkashifu kuwa hajui kuimba na kumwambia arudi nyumbani kwako Tandahimba kulima Ufuta na Korosho lakinii kumbe hawakujua  kumpiga chura teke ndiyo kumuongezea mwendo.

 

 MONDI ATAMANI UWEPO WA HARMONIZE

Ukifuatilia kwa makini utagundua tu hili kuwa Harmonize alikuwa kichwa . Tazama mashairi ya wimbo kama “I miss u” wa Diamond unauona kabisa uandishi wa Harmonize.

“Cheki na nyimbo zingine kabla ya Harmonize kuondoka, Leo unakuja kuimbiwa wimbo kama Gere melody mbaya , mashairi ya kawaida sana na ndio maana ulidumu kwa Siku tatu tu.

Angalia wimbo wa Jeje, Diamond mwenyewe hajui maana ya Jeje. Ndani ya wimbo Diamond anamini kuimba matusi ndio “kunam- bust” mashairi ya kitoto sana hayana maneno ya kumfikirisha mtu.

“ Rudi kwenye nyimbo kama “Baba Lao” au “Kanyaga”. Yaani mashairi ya kawaida sana sema wanayaforce masikio ya watu kuyasikiliza kwa muda mrefu dakika za mwisho zinaishia kuwa nyimbo za watoto.

“Nahisi uwepo wa Harmonize  pale ulikuwa na msaada mkubwa sana kwa Dimaond kiuandishi. Na ndio maana huyu Zuchu katoka kikawaida sana, kakosa mwandishi japo ni mkali sana wa kuimba.

“Amini nakwambia kama Harmonize angekuwa bado yuko pale Zuchu angetoboa mapema sana ila kwa sasa itabidi itumike nguvu kubwa sana kama iliyotumika kwa Mboso alafu watu wanakuja kumuelewa baadae.

Makala: Khadija Bakari

Leave a Comment