×

Juliana Lumumba: Ubelgiji Irejeshe Meno, Mifupa ya Baba

Juliana Lumumba, binti wa marehemu Patrice Lumumba.

JULIANA LUMUMBA, mtoto wa aliyekuwa waziri kuu wa kwanza wa nchi ambayo leo inajulikana kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Patrice Lumumba,  ameandika barua kwenda kwa Mfalme Philippe wa Ubelgiji akitaka nchi hiyo irejeshe meno na mifupa ya vidole vya baba yake aliyeuawa mwaka 1961, muda mfupi baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka katika ukoloni wa Ubelgiji.

 

“Sisi watoto wa Lumumba, sisi familia ya Lumumba tunataka  kurudishwa kwa mabaki ya Patrice Emery Lumumba katika ardhi ya wahenga wake,” inasema barua hiyo iliyonukuliwa katika vyombo vya habari.

 

Mabaki hayo yalihifadhiwa na mkuu wa zamani wa polisi wa Ubelgiji,  Gérard Soete, aliyekiri kwamba alisaidia katika mauaji ya Lumumba mwaka 1961.

Patrice Lumumba, aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Juliana Lumumba alituma barua hiyo Juni 30 mwaka huu (2020) siku ambayo inaadhimisha uhuru wa Congo.

 

Leave a Comment