×

Mama: “Sipendi Nandy Aingie Kwenye Ndoa” – Video

MAMA mzazi wa msanii  wa Bongo Fleva, Fausta Mfinanga, maarufu kama Nandy, ameweka bayana juu ya maamuzi ya mwanaye kufunga ndoa na msanii mwenzake, Bill Nas,  ambaye ni mpenzi wake wa muda mrefu sasa.

 

Akizungumza na Global TV Online wakati wa uzinduzi wa Nandy Bridal, mama Nandy amesema; “Siwezi kusema tumemkubali Bill Nas au tumemkataa, Nandy ni mtu mzima anachokifanya anakijua, kwa hiyo hatuwezi kumchagulia aolewe na nani, ni uhuru wake kuchagua.

 

“Lakini kwa sasa nisingependelea aingie kwenye mambo ya ndoa kwa sababu ana malengo yake, ana vitu vyake anavyotaka kuvifanya ili afikie mafanikio yake, kwa hiyo mimi naona angefanya kwanza kazi yake, haya mengine yatakuja,” amesema Mama Nandy.

 

Aidha, mama huyo ameongeza kuwa Nandy ni mtoto ambaye anamsikiliza sana, hivyo kama mzazi anajivunia kuwa na mtoto wa namna ile.

“Anajielewa, ana nidhamu na ananisikiliza sana, nikimwambia usifanye hivi hafanyi, anatukanwa sana mitandaoni lakini hajali wala hajibu chochote kwa sababu matusi ni sehemu ya mafanikio yake,” aliongeza mama huyo akizungumzia bifu la Nandy na Gigy Money.

 

Leave a Comment