×

Yanga Yatema Nyota 14 – Tshishimbi, Banka, Ngassa, Molinga…

YANGA Agosti 3, 2020 wametangaza nyota wake 14 waliowaacha huku mchezaji wao wa kigeni, Bernard Morrison, akiachwa kikosini kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ingawa bado kuna sintofahamu juu ya mkataba wake.

 

Wakati Morrison akibaki, nahodha wao Papy Tshishimbi, Mohamed Issa ‘Banka’, Mrisho Ngassa, David Molinga, Jaffary Mohammed, Tariq Seif, Andrew Vincent wao mikataba yao imemalizika hivyo wameachwa huru.

 

Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema Morrison bado wana mkataba naye.
“Morrison ni mchezaji wetu na ndiyo maana tukasema aende sehemu yoyote kusaini kama kweli anasema hana mkataba,” alisema Bumbuli.

Bumbuli amesema wachezaji Ali Mtoni, Ali Ali, Yikpe Gislain, Eric Kabamba, Rafael Daudi, Issa Maundu na Patrick Sibomana hawa wapo katika mazungumzo ya kusitishiwa mikataba ambao wamepeana muda wa wiki moja kuzungumza.

Wachezaji waliobaki kuitumikia Yanga ni Farouk Shikhalo, Ramadhani Kabwili, Metacha Mnata, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Morrison, Faisal Salum, Deus Kaseka, Ditram Nchimbi, Balama Mapinduzi, Abdulaziz Makame, Paul Godfrey, Adeyun Saleh, Said Juma Makapu.

 

Bumbuli amesema kuwa wakongwe Juma Abdul na Kelvin Yondani ambao mikataba yao imemalizika wanaendelea kuzungumza nao kwa ajili ya mikataba mipya.

Leave a Comment