
Mume wa mwanamuziki na mjasiliamali, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ Ashiraf Uchebe amesema kuwa anaendelea vizuri na biashara zake kama kawaida tofauti na watu walivyokuwa wakifikiria kubwa uenda hata biashara yake angefunga kutokana na kila mtu kumchukia, kisa madai ya kumpiga mkewe huyo.
Akizungumza na Risasi Jumatano,Uchebe alisema kuwa anamshukuru sana Mungu,anaendelea vizuri sana na biashara yake ya kila siku ingawaje watu wengi walidhani kuwa angeanguka au angefedheheka baada ya picha za za kipigo za mkewe huyo kusambaa kwenye mitandao na wengi kumchukulia mtu katili.
“ Mungu ni mwema sana, niko vizuri kulika hata jana na biashara yangu inaendelea vizuri kwasababu amnenipa uwezo wa kusimama vizuri kabisa japokuwa matatizo yalijitokeza lakini niko sawa nilijua watu wangeniona mimi mkatili na hata bidhaa zangu wangezisusa lakini wako pamoja na mimi bado nashukuru”alisema Uchebe ambaye hivi karibuni alikumbana na kashfa ya kumpiga mkewe huyo vibaya usoni mpaka kupekelea kutengana kwa sasa.
Na Imelda Mtema.