×

Zuchu Amburuza Tena Harmonize!

DAR: Memba mpya wa lebo kubwa ya muziki barani Afrika, Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman Sudi ‘Zuchu’, amemburuza bosi wa Lebo ya Konde Music Worldwide, Rajab Abdul ‘Harmonize’ au Harmo kwa mara nyingine.

 

Zuchu na Harmo wametengeneza rekodi ya ngoma ambazo zimefanya vizuri kwa mwezi Julai, mwaka huu kwenye Mtandao wa kusambaza na kuuza muziki wa Spotify huku wakiambatana na wasanii wengine ambao nao wameingia kwenye orodha hiyo.

 

Kwenye Mtandao wa Spotify, Zuchu ameongoza kupata wasikilizaji wengi zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki kupitia wimbo wake wa Mauzauza uliopo ndani ya Extended Play (EP) yake kama alivyofanya awali ambapo alimkimbiza jamaa huyo kupitia Mtandao wa YouTube, na sasa ni kupitia Spotify.

 

Mauzauza ni wimbo ambao Zuchu amemshirikisha mama yake mzazi ambaye ni mwanamuziki mkongwe wa Taarab, Malkia Khadija Omari Kopa. Katika orodha hiyo, Harmo ameburuzwa mpaka nafasi ya sita na wimbo wake wa Mpaka Kesho ambao nao umekuwa ukifanya vizuri kwenye mitandao mingine.

 

Orodha hiyo ya ngoma bora za Julai, mwaka huu ilikuwa ikiangalia EP au album za wasanii mbalimbali wa Afrika Mashariki waliofanya vizuri.

 

Wasanii wengine waliofanya vizuri kwenye orodha hiyo ni pamoja na Maya Amolo wa nchini Kenya aliyeshika nafasi ya pili na ngoma yake ya Lush Green. Nafasi ya tatu imekwenda kwa Vinka kutoka Uganda na ngoma yake ya Love Panic.

 

Nafasi ya nne imekwenda kwa Kahush, Chris Kaiga wa Kenya na ngoma yake ya Mastingo. Nafasi ya tano imekwenda kwa Spice Diana kutoka Uganda na ngoma yake ya Kokonya akiwa na Harmonize.

 

Zuchu amekuwa ni msanii ambaye ameweka rekodi nzuri kwenye muziki wake tangu kutambulishwa kwake, Aprili 8, mwaka huu, kwani EP yake imesheheni ngoma kali na zote zimefanya vizuri kwa kusikilizwa kwenye mitandao ya kupakua muziki ikiwemo Spotify na Boom Play.

 

Mbali na hilo, Zuchu ameweza kufi kisha watazamaji milioni kumi kwenye Mtandao wa YouTube ndani ya kipindi cha miezi mitatu pekee.

Stori: Happyness Masunga. Ijumaa

Leave a Comment