×

Ndege ya India Yaanguka, Yaua Watu 18

NDEGE ya abiria ya Shirika la Air India aina ya Boeing 737 iliyokuwa na watu 190 imeanguka katika uwanja wa ndege wa Calcutta wakati ikitokea Dubai, usiku wa kuamkia leo na kuua watu 18 huku wengine 156 wakijeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya usalama wa anga nchini humo, inadaiwa kuwa ndege hoyo imeanguka wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa jimbo la Kusini mwa India, Kerala, baada ya kuzidiwa na upepo wa monsoon ambao ndiyo msimu wake kwa sasa.

Shughuli za uokoaji zinaendelea, huku huduma za dharura zikiwa zinaendelea uwanjani hapo licha ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati ndege hiyo inaanguka.

Bado haijafahamika kama kuna madhara yoyote yaliyotokea. Picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zimeonesha ndege hiyo iliwa imevunjika vipande viwili.

Tukio hilo limetokea mwendo wa saa moja kwa saa za eneo hilo kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha. Kumekuwepo na mafuriko na maporomoko ya udongo, wakati huu wa kipindi cha monsoon.

Leave a Comment