×

Basi la Digidigi Lapata Ajali Buchosa Wilaya ya Sengerema

Basi la abiria mali ya Kampuni ya Digidigi lililokuwa likitokea katika Kijiji cha Kahunda kwenda Mwanza Mjini limepata ajari leo asubuhi, katika kona ya barabara iliyopo karibu na mto unaotenganisha Kijiji cha Chamanyete na Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosa Wilaya ya Sengerema.

Kwa mujibu a mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa imetokea wakati dereva wa basi akijaribu kupishana na gari ndogo lililokuwa likitokea katika Kijiji cha Bupandwamela kwenda Kahunda.

Aidha, imeelezwa kuwa mtu mmoja amevunyika mguu na wengine (idadi haijafahamika) wamejeruhiwa ambapo wote wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

 

Leave a Comment