×

Kichapo Kitakatifu, Barca 2-8 Bayern

TIMU ya Bayern Munich imeiadhibu vibaya timu ya Barcelona na kuiondosha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kuitwanga bao 8-2 kwenye mechi ya Robo Fainali. Sasa wanaungana na Manchester City na Lyon kwenye nusu fainali.

Matokeo hayo ya kushindwa kwa Barcelona ni mabaya zaidi katika kushiriki kwake katika Ligi ya  Mabingwa katika mapambano huo uliofanyika jijini Lisbon, Ureno.

Thomas Muller alianza kuipatia bao Bayrn dakika za mwanzo kabla ya  David Alaba kusawazisha mchezo huo kwa kujifunga na kufanya mabao kuwa 1-1.

Bayern iliongeza bado kupitia kwa Ivan Perisic kupitia basi ya Srge Gnabry.  Muda mfupi baadaye Bayen walikuwa mbele kwa mabao manne, moja likifungwa na Gnabry na Muller.

Hata hivyo, Luis Suarez aliifungia timu yake bao la pili katika kipindi cha pili, lakini muda mfupi baadaye Kimmich alifunga bao na ubao wa mabao kusoma 5-2.

Bayern waliendeleza libeneke kupitia Robert Lwendowski aliyefunga bao kwa kichwa kupitia pasi ya Philippe Coutinho.

Barcelona 2, Bayern Munich 8 (FINAL)

⚽Bayern Munich: Thomas Muller (4′)
⚽Barcelona: David Alaba – OG (7′)
⚽Bayern Munich: Ivan Perisic (21′)
⚽Bayern Munich: Serge Gnabry (27′)
⚽Bayern Munich: Thomas Muller (31′)
⚽Barcelona: Luis Suarez (57′)
⚽Bayern Munich: Joshua Kimmich (63′)
⚽Bayern Munich: Robert Lewandowski (82′)
⚽Bayern Munich: Philippe Coutinho (85′)
⚽Bayern Munich: Philippe Coutinho (89′).

 

Katika matokeo hayo, Robert Lewandowski amefunga bao lake la 14 Kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, hii inamaanisha amefunga kwenye kila mechi ya #UCL msimu huu

Wakati huohuo, Barcelona inatarajiwa kumtimua kocha wake Quique Setien baada ya kupokea kipigo kizito cha mabao 8-2 mbele ya Bayern.

 

 

Leave a Comment