×

Mzee Chilo Aomba Vifaa vya JWTZ!

Dar: Mkongwe wa filamu za Kibongo, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo’ ameiomba Serikali kuwapatia wasanii majengo na vifaa vya Serikali ikiwemo vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuchezea filamu zao.

 

Mzee Chilo alimuomba ombi hilo Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alipokuwa akizindua kanuni mpya za Bodi ya Filamu Tanzania (BFT).

 

Katika ombi hilo, Mzee Chilo alimuomba Waziri Mwakyembe kwa nafasi yake awasaidie kibali ili waruhusiwe kutumia majengo ya Serikali kama hospitali, vituo vya Polisi, magereza, kambi za jeshi na vifaa vya kijeshi kama zifanyavyo baadhi ya nchi kama vile Marekani, ili kuleta uhalisia wa filamu zao.

 

“Tunaomba waziri utufikishie ombi la kuyatumia maeneo ya Serikali kama kambi za jeshi na vifaa vyake kama sare za kijeshi, bunduki, vifaru, mabomu pia hospitalini napo tupewe ruhusa ya kutumia vifaa vyake kama mashine za CT-Scan na nyinginezo, magereza, vituo vya Polisi na kwingineko,” alisema Mzee Chilo.

Kwa upande wake, Waziri Mwakyembe alilipokea wazo hilo na kuahidi kulifanyia kazi.

Stori: Richard Bukos. Ijumaa

Leave a Comment