Naibu Gavana wa BoT, Dk.Bernard Kibesse akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi benki ya Mwanga Hakika Microfinance Bank iliyotokana na muunganiko wa benki tatu ikiwamo Mwanga community Bank,Hakika Microfinance Bank Pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi, Eng.Ridhuan Mringo.Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk.Bernad Kibesse (kushoto), Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya(katikati) wakifuatilia zoezi la uzinduzi wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd.Benki hiyo ni muunganiko wa benki tatu (Mwanga Community bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank).Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd.Mteja wa kwanza kupata huduma kutoka benki mpya ya Mwanga Hakika Microfinance Bank,Gabriel Ndunga iliyozinduliwa jana baada ya kuungana kwa benki tatu ikiwamo Mwanga Community Bank, Hakika Microfinance Bank Pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank.Naibu Gavana wa BoT, Dk Bernard Kibesse (Kulia), Naibu Mwekezaji, Raymond Tarimo pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Mhandishi Ridhuan Mringo wakifurahi baada ya kuzindua benki mpya iitwayo Mwanga Hakika Microfiance Bank baada ya muunganiko wa benki tatu tatu (Mwanga Community bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank).Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Jagjit Singh.