×

Viingilio Simba Day Vyatajwa, Diamond Kuburudisha! -Video

AFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara,  leo Agosti 19, 2020,  amesema Simba itacheza na timu kutoka Burundi ya Vital’O katika kilele cha wiki ya klabu hiyo ijulikanayo kwa  ‘Simba Day’  siku ya Jumamosi Agosti 22, katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Manara amesema walipanga kucheza na Al Ahly lakini changamoto ya corona imefanya jambo hilo kuwa gumu.

“Tunaamini Vital’O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo,” alisema. 

Pia amesema siku hiyo ya Simba Day burudani itatolewa na Twanga Pepeta, Tunda Man, Meja Kunta, Mwasiti na Diamond Platinumz.

Viingilio kwenye sherehe na tafrija hiyo kenye Uwanja wa Uhuru itakuwa Sh. 2,000 na Uwanja wa Mkapa Mzunguko itakuwa 7,000/- VIP C 20,000/-,  VIP B 30,000/-,  VIP A 40,000/- na kutakuwa na tiketi maalum za Platinum 150,000/-

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment