×

Waliofariki kwa Covid-19 Kenya Wafikia 487

KENYA imetangaza watu wanne zaidi kufariki kutokana na CoronaVirus na kufanya idadi ya vifo kufikia 487. Aidha, watu 271 wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya CoronaVirus kutoka sampuli 4,019 na kufanya nchi hiyo kuwa na jumla ya watu 30,636 waliothibitika kuwa na maambukizi.

 

Katika waliothibitika kuwa na maambukizi ni pamoja na mtoto wa mwaka mmoja. Pia 178 kati yao ni wanaume huku 93 wakiwa ni wanawake. Watu 208 wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufikia 17,368.

 

 

Leave a Comment