MASTAA wapya waliosajiliwa na Simba juzi waliteka mazoezi ya timu hiyo walipoanza kufanya kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Simba ilianza program ya mazoezi chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Sven Vandenbroeck na msaidizi wake Selemani Matola aliyewahi kuichezea Simba.
Katika mazoezi hayo, wachezaji wa zamani waliokosekana ni Pascal Wawa, Luis Miquissone, Francis Kahata, Meddie Kagere, Clatous Chama na Shomari Kapombe.
Mastaa wapya waliosajiliwa na kuanza mazoezi ni Chris Mugalu, Larry Bwalya, Bernard Morison, Joash Onyango, Charles Ilanfya, David Kameta ‘Duchu’ na Ibrahim Ame ‘Verane’.
Timu hiyo ilifi ka uwanjani hapo na kuanza mazoezi saa 10:20 jioni na program ya kwanza kuanza kuifanya ni kunyoosha viungo iliyokuwa inaoongozwa na kocha wa viungo, Adel Zrane.
Baada ya kumaliza program hiyo, haraka wakahamia katika kupiga pasi fupi na wachezaji waligawanywa kwa makundi wakiwa wanne na kupigiana pasi kwa mitindo tofauti katika kurejesha umakini wa upigaji wa pasi.
Program hiyo ilitumia dakika kumi pekee.Wakiendelea na program hizo chini ya Adel, wachezaji wote walionekana kufanya vema huku Bwalya na Morrison wakionekana kupiga pasi kwa mbwwembwe na kiufundi.
Morisson alionekana kupiga pasi kwa nguvu na alikuwa akifanya hivyo kwa wachezaji wenzake kama masihara huku mashabiki wakihoji kwa nini kiungo huyo anapiga pasi hivyo.
Baada ya kumaliza program hiyo, wakatenganishwa makundi na kati ya hayo lilikuwepo kundi lililokuwa linakimbia mbio ndefu likiongozwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.
Kundi lingine lilikuwa ni lile la kukimbia mbio fupi lililokuwepo katikati ya uwanja wakikimbia kwa kuzizunguka koni zilizokuiwa zimepangwa na kocha Adel.
Wakati mbio hizo zikiendelea, mashabiki waliofi ka kufuatilia mazoezi hayo walitegemea kuwaona mastaa wapya Bwalya, Mugalu na Morisson wangechemka lakini walifanya mazoezi mwanzo mwisho tena kwa ufasaha kabisa.
Walipomaliza program hizo za mbio, wakahamia kwenye kuuchezea mpira kwa kutumia viungo vyote kichwa, miguu, kifua na mapaja hapo ndiyo Bwalya alipoanza kuonyesha mbwembwe zake mashabiki waliofurika kuliko kipindi chochote mazoezini hapo walilipuka kwa shangwe kwenye kila tukio.


