×

Shigongo: Buchosa Tuvunje Makundi, Wa-TZ Tumpe Kura JPM – Video

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Buchosa, Sengerema mkoani Mwanza, Eric Shigongo amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuacha chuki za kisiasa na badala yake kuunganisha nguvu kwa pamoja na kushirikiana ili chama hicho kipate ushindi na hatimaye maendeleo katika eneo hilo.

 

Shigongo amesema hayo leo Ijumaa, Agsoti 28, 2020 wakati akizungumza na wananchi hao na Watanzania wote kupitia Global TV Online na +255 Global Radio huku akiwaomba Watanzania wote kukichagua CCM na Mbombea wake wa Urais ambaye ni Dkt. John Pombe Magufuli ili aendelee kufanya makubwa zaidi ya aliyofanya miaka mitano iliyopita katika awamu yake ya kwanza ya uongozi.

 

“Ninawashukuru sana Wana-Buchosa kwa mapenzi yenu, ninawashukuru Watanzania wote, hakuna kipindi ambacho nimepokea simu nyingi za kunipongeza kama sasa. Nikishukuru chama changu CCM chini ya Mwenyekiti wetu Dkt. Magufuli kwa kuniamini nipeperushe bendera ya chama.

 

“Naamini Baba na Mama wanafurahi sasa hivi huko Mbinguni kuona mtoto wao ninafanya kitu ambacho walitamani nikifanye wakiwa hai. Mwaka 2005 baba aliniita wazee wa Buchosa walikuwa wamemfuata wakiniomba nikagombee lakini sikudhani kama ningeweza kuwa mwanasiasa.

 

“Naamini Baba na Mama wanafurahi sasa hivi huko Mbinguni kuona mtoto wao ninafanya kitu ambacho walitamani nikifanye wakiwa hai. Mwaka 2005 baba aliniita wazee wa Buchosa walikuwa wamemfuata wakiniomba nikagombee lakini sikudhani kama ningeweza kuwa mwanasiasa.

 

“Dkt. Kikwete alikuja kwenye kampeni 2010 akanipandisha jukwani kijijini Nyehunge, akaniambia Eric wewe bado kijana mwache mwenzako alitumikie Taifa, nilikubali na nikampigia kampeni Dkt. Tizeba akashinda, 2015 nilimwachia sikuchukua fomu wala kushiriki uchaguzi.

 

“Mwaka 2020 nikasema ni wakati wa kutimiza ndoto ya wazazi wangu, siku ya uchaguzi wajumbe wakatupigia kura, mimi na mwenzangu Dkt. Tizeba wakatupa idadi sawa ya kura 345 kila mmoja wetu, tukasubiri na mwisho wa siku nikateuliwa na Chama changu.

 

“Ninajua Wana-Buchosa mna matarajio makubwa na mimi, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu na Mungu anisaidie niweze kuwatumikia vile inavyotakiwa, nifanye jambo ambalo mwisho wa siku watu waseme alikuwepo mtu anaitwa Shogongo alifanya jambo hili.

 

“Inawezekana kabisa kwa kushirikiana na wananchi tukafanya mabadiliko makubwa kwenye maeneo yetu. Ninawasihi wanabuchosa tuondoe makundi, tuwe kitu kimoja, tuachane na tofauti zetu, tuunganishe nguvu zetu, tushinde uchaguzi, hatuwezi kushinda tukiwa tujegawanyika.

 

“Tuondoe chuki, siasa zisitugawanye, siasa zituunganishe, hakuna maendeleo tukiwa tumegawanyika. Kunzia leo nimewasamehe wote walionipiga vita, nitafanya kazi na mtu yeyote, wa kwanza nitakayefanya nae kazi ni Dkt. Tizeba, migawanyiko inatuchelewesha.

 

“Ninawaomba Watanzania wote kesho tufurike pale Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kwenye uzinduzi wa kampenzi za CCM, tukamsikilieze Mhe. Magufuli anachotuelekeza, mambo ambayo CCM imepanga kuyafanya kwa miaka mitano iwapo itapewa ridhaa ya kuendelea kuiongoza nchi.

 

“Mimi nina imani kubwa sana na Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa mambo aliyoyafanya ndani ya miaka mitano na Watanzania mmeshuhudia, nchi yetu imeweza kutoka kwenye uchumi wa chini hadi uchumi wa kati, siku ya kesho ni muhimu sana kwa Watanzania.

 

“Tunapofanya uchaguzi tunachagua maisha yetu, ni lazima tunagalie tunamkabidhi nani maisha yetu, hakuna majaribio katika kuchagua viongozi, lazima tuchague mtu ambaye tunaamini atatufanyia makubwa, na Magufuli pekee ndiye anayefaa.

 

“Tanzania lazima tuwe na usawa, kila mtu awe na nafasi sawa na mwingine, Mhe. Magufuli amefanya makubwa, reli, ndege, umeme, afya, maji, barabara, inaonyesha alivyo na uchungu na maendeleo ya Tanzania.

 

“Magufuli ana nia njema na nchi yetu, tumpe miaka mingine 5, sioni mwingine wa kumkabidhi taifa hili, si kwamba wengine nawadharau hapana, naangalia historia ya mtu ili nifanye maamuzi, Magufuli ni mwaminifu, mtiifu, hana tamaa, JPM ni picha halisi ya Mwl. Nyerere.

 

“Nafahamu Buchosa tunazo changamoto nyingi sana, barabara, afya, maji, elimu, hatuna chuo hata kimoja cha ufundi, high school moja, haya ni baadhi ya mambo yaliyonisukuma nikaonyeshe uongozi maana yake nini, hakuna maendeleo bila uongozi bora.

 

“Si kwamba nchi inajengwa na watu wakubwa tu, mwalimu wa shule ya msingi, mama muuza ndizi, muuguzi anayechoma watoto sindano, mkulima na wananchi wengine wa kawaida ndiyo wanajenga nchi yetu.

 

“Tusichague viongozi kwa majaribio, tutajuta miaka mingi sana, nchi hii inajengwa kila sehemu kwa fedha zetu za ndani, Mhe. Magufuli ameleta nidhamu ya fedha, maendeleo kila eneo, tunataka nini Watanzania, tuwe na imani na CCM, hii ni CCM mpya kabisa.

 

“Mhe. Magufuli kwa sababu ametokea chini mpaka akafika juu, ni mtoto wa maskini anayejua maana ya kulala njaa, anafahamu shida na matatizo yote ya Watanzania kwa sababu ameyapitia, amedhamiria kuibadili Tanzania, tumuungeni mkono.

 

“Nataka Buchosa iwe kama ya akina Mzee Lulegula, akina Mzee Shindika, Chitalilo, hakukuwa na makundi, tuyaondoe makundi haya, lazima yaondoke, tuache chuki za siasa, ibaki CCM moja tupate ushindi wa maisha yetu, ninawahakikishieni kwamba sitawaangusha.

 

“Kwa neema ya Mungu aliyonipa nina biashara zangu Kigamboni hapa Dar, ningeweza kugombea Kigamboni, au Temeke, au Kinondoni, au Nyamagana, au Ilemela, lakini nikaamua kuchagua Buchosa kwa sababu nina mapenzi makubwa na Wana-Buchosa ambako ndiko nilikotoka.

 

“Ninaacha kila kitu ninaenda kushughulikia matatizo ya wananchi wenzangu, ndugu zangu nimeamua kugombea ubunge kwa sababu watu wangu wanahitaji kiongozi aliye bora kuwasaidia, nitaifanya kazi hii kwa uaminifu mkubwa, ninamuomba Mungu na atasimama nasi,” amesema Shigongo.

 

MSIKILIZE SHIGONGO

Leave a Comment