×

Breaking: Yanga Yatangaza Kocha Mpya, Rekodi Yake Inatisha

KLABU ya Yanga ya Dar es Slaaam imemtangaza Zlatko Krmpotić raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 62 kuwa kocha wake mkuu akitokea Polokwane City FC ya Afrika Kusini (ambayo alimaliza nayo mkataba mwaka Novemba 2019), ambapo amesaini kwa mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania.

 

Zlatko ambaye amewahi kushinda Kombe la Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) akiwa na TP Mazembe ya DRC, anachukua nafasi ya Luc Eymael ambaye ametimuliwa na klabu hiyo mwishoni mwa msimu uliyopita.

 

Akimtangaza kocha huyo, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambaye ndiye anashughulika na masuala ya usajili wa wachezaji wa llabu hiyo ya Jangwani, Eng. Hersi, amesema leo Agosti 28, 2020 kuwa Zlatiko atatua nchini kesho kuanza kazi rasmi. Hii ni baada ya kuachana na kocha Mrundi, Cedric Kaze, ambaye ameshindwa kutua nchini kutokana na sababu za kifamilia.

 

UZOEFU
Jina Kamili Zlatko Krmpotić
Tarehe ya Kuzaliwa 7 August 1958 (age 62)
Eneo Alipozaliwa Belgrade, FPR Yugoslavia
Urefu 1.79 m (5 ft 10 12 in)
Nafasi Aliyocheza (s) Defender
Akiwa Kijana
Red Star Belgrade
Akiwa Senior
Mwaka Timu Apps (Gls)
1977–1986 Red Star Belgrade 180 (7)
1986–1988 Gençlerbirliği 60 (3)
AIK Bačka Topola
Jumla 240 (10)
Timu ya Taifa
1978 Yugoslavia U21 5 (0)
1980–1982 Yugoslavia 8 (0)
Timu Alizofundisha
AIK Bačka Topola
1994–1996 Degerfors IF
1997–1998 Sloga Jugomagnat
1999 Ankaragücü
1999–2000 OFK Beograd
2000 Obilić
2001 Paniliakos
2001 Nea Salamis
2002 Kairat
2005 Serbia and Montenegro U17
2005–2006 Kazma
2007–2008 Serbia U19
2013 OFK Beograd
2014 OFK Beograd
2015 TP Mazembe (assistant)
2016 Don Bosco
2017 ZESCO United
2018 Jwaneng Galaxy
2019 APR FC
2019 Polokwane City

Red Star Belgrade

  • Yugoslav First League: 1979–80, 1980–81, 1983–84
  • Yugoslav Cup: 1981–82, 1984–85
Club Domestic
Super League Winner 1x 2017
Cup Winner 1x 1986/1987
Super Cup Runner-up 1x 1987/1988

International

Yugoslavia
  • UEFA Under-21 Championship: 1978

Honors

  • Best coach of the Democratic Republic of Congo championship 2016-2017
  • Best coach of Zambian Superleague 2017-2018
  • Best coach of Botswana Premier League 2018
  • Best coach of Africa 2017-2018.

Leave a Comment