CHUO Kikuu cha Namibia, kitengo cha dawa ya mifugo, kinawafundisha mbwa kubaini virusi vya corona kwa kunusa. Mpango wa nchi hiyo ni kuwapeleka mbwa hao katika viwanja vya ndege na vituo vya mpakani, kwa mujibu wa mtandao wa The Namibian.
Mbwa wamethibitishwa kuwa na uwezo wa kubaini virusi vya corona kwa asilimia 95, mhadhiri wa somo la tiba ya wanyama, Alma Raath, amesema.
Mradi huo ulianzishwa miezi miwili iliyopita, inasema taarifa ya mtandao huo wa The Namibian, lakini haujataja ni lini mbwa hao watakuwa tayari kufanya kazi.
Mtandao huo unasema nchi hiyo itakuwa ya kwanza duniani kutumia mbwa kubaini virusi vya corona.
