WAKATI nchi nyingine zikiwa chini ya lock-down kupisha janga la homa inayoambukizwa na virusi vya corona — Covid-19 — nchini Thailand pamebuniwa mgahawa unaofanana na ndege, lengo ni kufanya watu hasa wasafiri kujiona kama wapo ndani ya ndege kipindi hiki cha lockdown.
Katika migahawa hiyo inayojulikana kama “migahawa ya kwenye ndege”, wateja hujiburudisha kwa kunywa kahawa katika jiji la Pattaya lililoko pwani ambapo hujiona kama vile wako kwenye ndege angani ambapo huduma zote kama zinazopatikana kwenye ndege hutolewa.
“Ndani ya huu mgahawa najiona kama nipo angani, kuna hadi sehemu ya daraja la kwanza, ” anasema mmoja wa wateja wa mgahawa huo.
“Katika mgahawa huu naweza kukaa sehemu ya daraja la kwanza na kuzunguka sehemu zote zinazofanana na zile zinazoongezea ndege, nikijifanya kama vile rubani wa ndege,” anasema Thipsuda Faksaithong (26) akiliambia shirika la habari la AFP.
Thailand ilikuwa nchi ya kwanza nje ya China kukumbwa na janga hilo la corona na hadi sasa imerekodi visa 3,400 vya watu waliopatwa na ugonjwa huo, wakati vifo ni 58.


