MKALI wa masauti, Christian Bella, ametangaza ujio wa albamu yake mpya ambapo kila siku kuanzia leo ataachia video na wimbo mpaka siku ya uzinduzi.
Katika hatua nyingine amesema licha ya ukimya wake, yeye ni msanii kati ya wasanii watatu wa Tanzania ambayo wanakubalika na kufanya shoo nyingi na kwamba ataachia video moja kila siku kwa siku tano mfululizo.
Aidha, amezungumzia ghorofa zake mbili ambazo amezijenga huko Mbweni jijini Dar es Salaam. Amesema baada ya ku-post clips ya mjengo huo, kuna watu wengi wanamwuuliza kwa nini anamiliki nyumba Tanzania wakati yeye ni raia wa Congo.
Tazama video iliyopo chini:
