MAOFISA wawili wa polisi wamepigwa risasi huku maelfu ya watu wakiandamana katika mji wa Louisville nchini Marekani baada ya jopo la mahakama kuamua kwamba hakuna mtu atakayeshtakiwa na mauaji ya mwanamke mweusi, Breonna Taylor.
Taylor, 26, alipigwa risasi mara kadhaa baada ya polisi kuvamia nyumba yake iliyopo Lousville, Machi 13, 2020 ambapo Brett Hankison na wenzake walikamatwa lakini baadaye mahakama imesema hakuna mtu atakayeshtakiwa kwa mauaji hayo.
Naibu afisa mkuu wa polisi, Robert Schroeder, amesema hali za polisi waliopigwa risasi zinaendelea vizuri.

