×

Mwili wa Mtoto wa Mfanyakazi wa Global Group Wazikwa Dar

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akishiriki kufukia udongo kwenye kaburi la mtoto wake Azizi Hasim leo katika makaburi ya makuburi, Ubungo Dar.

Meneja wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho, leo Jumapili ameongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo katika kumfariji mfanyakazi mwenzao, Hashim Aziz, ambaye jana Septemba 27, 2020 alifiwa na mtoto wake katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.  Mtoto huyo amezikwa leo katika Makaburi ya Makuburi jijini Dar es Salaam, waombolezaji mbalimbali walijitokeza wakiwemo wafanyakazi wenzake Aziz.

 HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

…Meneja wa Global, Abdallah Mrisho akimpa pole Aziz Hashim baada ya kumzika mwanaye leo kwenye Makaburi ya Makuburi, Ubungo.
…Baadhi ya wafanyakazi wa Global wakiwa mbele ya kaburi la marehemu leo baada ya kumzika.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Sifael Paul akishiriki kumzika mtoto wa Azizi Hashim kwenye Makaburi ya Makubiri, Ubungo leo.
…Mhariri Kiongozi, Richard Manyota (mwenye fulana ya njano) akishiriki mazishi.

Leave a Comment