×
Global Publishers
  • Home
  • Habari
    • Kimataifa
    • Kitaifa
  • Global TV
  • Magazeti
  • Ajira
  • Burudani
    • Audio Music
    • Music Videos
    • Dar Live
  • Michezo
  • Makala
    • Afya
    • Mahaba & Maisha
    • Burudani
    • Hadithi
    • Mikasa
    • Siasa
  1. Home
  2. Celebrities
  3. John Legend, Mkewe Wapata Pigo

John Legend, Mkewe Wapata Pigo

Global Publishers October 1, 2020 4,586 views 0 Comments
SHARE THIS:

FAMILIA ya mwanamuziki maarufu duniani kutoka nchini Marekani, John Legend (41) wamepata pigo baada ya kumpoteza mtoto wao waliyemtegemea kumpata ambaye tayari walikuwa wamempa jina la Jack.

 

Kupitia kwenye Instagram ya mke wa John Legend, Chrissy Teigen (34) ameandika ujumbe mzito kuhusu kutokea kwa jambo hilo ambapo amesema kilichosababisha mtoto wao kufariki ni baada ya kuvuja damu nyingi lakini haijaelezwa kama amefariki akiwa tumboni ama baada ya kujifungua.

Tangu mwanzo wa ujauzito wake, Teigen amekuwa akielezea hali yake ya ujauzito kwenye social media. Mwezi uliyopita alielezea namna alivyokuwa akihangaika na ujauzito wake huo ambao aliupata kwa njia ya kawaida tofauti na ujauzito wa watoto wake wakubwa wawili (Luna miaka 4 na Miles miaka 2) ambao aliupata kwa njia ya kupandikiza (in vitro fertilization – IVF, mnamo Aprili 2016 na May 2018).

 

Alieleza pia kuwa alikuwa akisumbuliwa na kichwa, kulegea kwa mishipa ya damu hali ambayo ilikuwa inamfanya kukosa nguvu mara kwa mara. Pia mishipa ya ukuta wa mimba ilikuwa imelegea, hali iliyosababisha kupasuka sababu ya pressure kubwa na kusababisha damu nyingi kuvuja. 

Hata hivyo amewashukuru wote ambao wamekuwa naye pamoja katika kipindi hiki kigumu akiwemo mwanamitindo maarufu duniani, Kim Kardashian, ambaye amekuwa naye pamoja mwanzo mpaka mwisho katika tatizo.

 

SHARE THIS:
Previous Next

Related Posts

NDOA KUMBADILI DINI SISTER FEY - Global Publishers BURUDANI

NDOA KUMBADILI DINI SISTER FEY

September 12, 2018
DILI ZA ZARI BAADA YA DIAMOND PLATNUMZ USIPIME - Global Publishers BURUDANI

DILI ZA ZARI BAADA YA DIAMOND PLATNUMZ USIPIME

October 29, 2018
Posts za Mastaa Diamond, Mwana FA, Vee Money Msiba wa Mzee Mengi - Global Publishers CELEBRITIES

Posts za Mastaa Diamond, Mwana FA, Vee Money Msiba wa Mzee Mengi

May 2, 2019
Esma: Diamond, Tanasha ndoa kama kawa! - Global Publishers BURUDANI

Esma: Diamond, Tanasha ndoa kama kawa!

April 19, 2019

Leave a Comment Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

DAKTARI

GLOBAL TV Online




SIMBA
YANGA
NEWS
Global Publishers
  • About Us
Download on the App Store
Get it on Google Play

© 2026 Global Publishers. All Rights Reserved.

Designed by Yatosha Web Services