×

Wahitimu Victory Secondary Walivyoonesha Umahiri Katika Ujasiriamali

Wahitimu hao wakiwapa zawadi viongozi wa meza kuu baadhi ya bidhaa walizotengeneza.

Wahitimu wa Shule ya Sekondary ya Victory iliyopo Vikindu mkoani Pwani wameonesha umahiri wao katika somo la Ujasiriamali ambalo walifundishwa sambamba na masomo mengine.

Umahiri huo waliuonesha kwenye mahafali ya 17 ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo.

Akizungumza kwenye mahafali hayo Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Peter Mtembei amesema wanafunzi hao sambamba na masomo ya taaluma kama sekondari nyingine wamekuwa wakifundishwa elimu ya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kimaisha baada ya kumaliza masomo yao.

“Katika ujasiriamali huo wataweza kutengeneza bidhaa mbalimbali na wanaweza kujiendeleza kwa kuanzisha viwanda vikubwa vya kuzalisha bidhaa hizo”. Amesema Mutembei.

Miongoni mwa bidhaa walizofundishwa kutengeneza na kuzionesha kwenye mahafali hayo ni pamoja na sabuni za maji, za kuoshea vyombo, mafuta, dawa za kusugulia vyoo bidhaa zote hizo zikiwa na nembo ya shule Victory ambayo ndio lebo ya shule yao.

Baada ya kuonesha bidhaa hizo waliwakabidhi viongozi wa meza kuu pamoja na waalikwa wengine kama zawadi yao na kuwaaga.

Akiwaaga wahitimu hao Mutembei ambaye anamiliki shule za St. Mark’s, Victory, Ujirani na St. Mathew Peter Mtembei amesema elimu hiyo ni muhimu sana katika ulimwengu wa kisasa.

“Ujasiriamali ndiyo kila kitu katika ulimwengu wa kisasa ndiyo maana hata nchi zilizoendelea nyingi zimebadili mfumo wa kielimu na kuongeza mkazo kwenye ujasiriamali ambao ndiyo ukombozi katika maisha ya kujitegemea”. Alisema Mutembei.

Sambamba na ujasiriamali Mutembei alisisitiza suala la nidhamu kwa wahitimu hao na kuwaambia kuwa duniani hakuna mafanikio bila nidhamu.

“Mkitoka hapa tunaomba mkaendeleze maadili mliyofundishwa na walimu wenu vinginevyo msije mkajikuta mnaishia kwenye utumiaji wa dawa za kulevya”. Alimaliza kusema mkurugenzi huyo.

Leave a Comment