JINO kwa jino kati ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi na Ali Kiba ‘King Kiba’ siyo uadui, ni uhasimu wa kimuziki ambao kwa sasa umefikia patamu.
Nani mkali wa Bongo Fleva na mfalme wa muziki huo Bongo baina yao; ndiyo chachandu lenyewe lililopo mitandaoni kwa mashabiki wa kambi hizo mbili.
“Mfalme wa Bongo Fleva ni Mondi,” shabiki mmoja anaandika mtandaoni; lakini King Kiba kupitia wimbo wake wa Mediocre, anajibu mapigo: “Yeaaaaah yeeeiyeee, pluu mpaka chini –PIGO, Unataka U-King na Mafundo, Mimi ndiyo BABA… Kingdom…. Kingdom.”
Akimaanisha mfalme ni yeye! Kando na shoo za majukwaani ambazo zamani zilikuwa ndiyo ulingo wao wa: “Ashuke au apande na aendelee au asiendelee.”
Siku hizi Mondi na King Kiba wanakutana mjini You Tube kwenye ma-video na maaudio. Juzi kati, Mondi akishirikishwa na Zuwena Othman ‘Zuchu’ katika ngoma ya Cheche na Litawachoma, akakichafua YouTube kwa kushika trending za juu kwa siku kadhaa.
Huo alikuwa ana-trendi na video ikionesha anaogelea kwenye bwana la kisasa ‘Swimming Pool’ na mwanadada mkali ambaye pia ni msanii, Mimi Mars. Mashabiki wa Diamond walipoanza kujimwambafai kwamba msanii huyo ndiyo mfalme Bongo, King Kiba akaibuka na kuwauliza “mnasemaje?”
Fasta akafyatua kombora la wimbo wa Mediocre uliojaa mashairi yenye madogo mazito akayatupa gizani kwa mistari kama hivi: You call me Kibaka, They call me King Kiba, Baba Keyaan, Toto la Mama Kiba, Njaa mi nashiba, unaishi kwa kuniiga, And I’m Alright, Ushamba mwiko kwa mtoto wa Kariakoosi Chezi na dada zangu, nacheza na dada ako.”
Wakati King Kiba akiachia pini hilo na kuushusha wimbo wa Cheche, You Tube, Mondi wakati Kama kakurupushwa, Mondi alipoona ametolewa kwenye ufalme mjini YouTube, alijampu kininja na kuachia video ya Litawachoma, aliyoshirikishwa na Zuchu na kuanza kumkimbiza King Kiba amshushe kitini, ndiyo maana tunasema ni jino kwa jino.
Asikuambie mtu, mitandaoni kutamu bwana! Muda mfupi tu baada ya video ya Litawachoma kuachiwa, komenti zikawa: “Ali Kiba imba sana, Ila domo (a.k.a ya zamani ya Mondi) akija, anakuja na kelele zake anasomba kijiji.” Watu weweeee!
Mara mashabiki wa Kiba wakasikia kelele; wakaja na makomenti ya kukera: “Kiba ndo King wa muziki wa Bongo Fleva hatabiriki, Hit baada ya hit, hakuna kucopycopy, ma idea yamejaa.”
Vipi hapo; ungekuwa wewe ndiyo hakimu ungempa nani ushindi kati ya Mondi na King Kiba, Risasi Jumatano tumeishia kusema: “Ni jino kwa jino, bampa tu bampa kati yao.”
STORI MWANDISHI WETU, RISASI
