×

Kalebezo Yaitikia! Shigongo Achanja Mbuga, Hakamatiki Buchosa

 

 

 

UMATI wa wananchi wa Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Kalebezo,  wamefurika kumpokea mgombea ubunge Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, alipofika kwa ajili ya mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoni kijijini hapo.

 

Akizungumza na wananchi katika mkutano huo, Shigongo amesema upendo waliomuonyesha wananchi wa Kalebezo ni upendo mkubwa sana kwake hivyo endapo atapewa ridhaa hiyo, basi yeye atawalipa utumishi ulio bora kwa kuwaletea maendeleo thabiti kwenye kata hiyo.

 

 

Shigongo amewasihi wananchi hao kuendelea kushirikiana kwa pamoja na kuachana na makundi ya kisiasa hasa kwa wanachama na wafuasi wa CCM ambayo yanaweza kukwamisha ushindi wa kishindo katika uchaguzi hapo Oktoba 28, mwaka huu.

 

 

Aidha, amesisitiza kutokuwa na chuki na watu wenye itikadi ya vyama vingine vya siasa kwani sote ni Watanzania na lengo kubwa ni kujenga nchi pamoja na kulinda amani na utulivu uliopo katika taifa la Tanzania.

 

 

Shigongo anaendelea na kampeni zake jimboni Buchosa akinadi sera za chama chake cha CCM pamoja na kuwaomba ridhaa wananchi ili wawachague viongozi wa CCM kuanzia kiti cha urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

 

 

 

Leave a Comment